Mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu katika kaunti ya Uasin Gishu la Center for Human Rights and Democracy Kipkorir Nge’tich ameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuwahakikishia wakenya uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 9 wa Huru na haki.
Akiongea afisini mwake Mjini Eldoret, mkurugenzi huyo alisema wakenya wanayo haki ya kuwachagua viongozi wanaowaenzi bila ya haki yao ya kidemokrasia kuhujumiwa.
Nge’tich vilevile alimtaka mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati kutokubali kuadahiwa Kwa kushiriki visa vya udanganyifu kwenye uchaguzi huo na kuliongoza taifa Kwa uchaguzi huru.