Baraza la wazee katika kaunti ya Uasin Gishu walipuuzilia mbali madai kwamba kaunti hiyo linaweza kuwa na vurugu wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 9 mwaka huu.
wakiongozwa na mwenyekiti wao Alex Mursi walidokeza kwamba wakaazi wa kaunti ya Uasin Gishu wamekuwa watu wa kukumbatia amani na wanashangaa sana kupata ujumbe kutoka kwa tume ya uwiano na utangamano NCIC kwamba kaunti liko kwa hali hati hati ya kiusalama wakiwataka wenyeji kuendelea na kudumisha amani hiyo.
Wakiongea na wanahabari mjini Eldoret,wazee hao wamedokeza kuwa kila mwaniaji kiti chochote cha kisiasa anayo haki ya kuendeleza kampeni zao katika kaunti nzima ya Uasin Gishu kwa wanachosema watapokelewa vyema na wauze sera zao kwa njia salama,ya heshima na kuacha kuwachochea wengine.
Hata hivyo,wazee wao walizitaka vyombo vya habari kutoa ripoti zao kwa njia isiyoegemea upande wowote wa kisiasa ndipo wakenya waweze kuelimika na amani iweze kudumishwa.
