Mti alioupanda Askofu Korir sasa una matunda

Jimbo katoliki la Eldoret limeandaa kumbukumbu ya tisa ya askofu mwendazake Cornelius Korir.

Askofu wa Jimbo katoliki la Kapsabet John Lelei akihubiri katika maadhimisho hayo kwenye kanisa la moyo mtakatifu wa yesu kathedali amemmiminia sifa katika ujasiri wake wa kuleta amani katika bonde la Kerio akisema alama za amani alizoacha kamwe hazitafutika nyoyoni mwa wakristu wa maendo hayo.

Amesema kuwa askofu Korir alihudimia taifa katika ulingo wa kisiasa kwa kuwapatanisha viongozi waliokuwa wakizozana hata katika mipaka mbalimbali mwa nchi.

Askofu Lelei amesema kuwa Korir alikuwa mtu wa Sala akitoa wito kwa Kila mkristu kuiga mfano wa askofu Korir.

Kulingana na askofu Lelei ni kuwa Korir alikuwa na moyo wa huruma kwa kuwakimbatia Kila mmoja bila kuwa na mipaka akitoa wito kwa Kila mmoja kuendeleza ruwaza ya kuleta amani na upatanksho miongoni mwa jamii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *