Tume ya uajiri wa umma imepuuzilia mbali dhana kuwa nafasi za ajira zilizoko nchini ni ya wachache na kutoa wito kwa vijana kujitokeza kutafuta nafasi hizo za ajira.
Naibu katibu kwenye tume hiyo Jackline Manani alisema kuwa hatua ya kuajiri inatolewa kwa njia ya uwazi bila kuwabagua wale walio na changamoto za kimaumbile katika nafasi zilizopo.
Tume hiyo ilitoa hamasa kwa vijana kujitokeza kutafuta nafasi hizo kwa kuwa mahojiano hayo yanafanywa kwa njia ya uwazi ili kuafikia wale ambao wamehitimu kwenye nafasi hizo.