Sita kwisha yaja mapya

Askofu mkuu mwandamizi mteule Dominic Kimengich amemkabidhi askofu John Lelei wadhifa wa uenyekiti wa Shule ya upili ya wasichana ya St Joseph Chepterit.

Akihubiri katika maadhimisho ya Misa ya shukrani kwenye shule hiyo askofu ametoa wito kwa watahiniwa kwenye shule hiyo kutia bidii na kuiga mfano wa mtakatifu Yosefu aliyejitolea katika maisha yake na hatimaye kuleta ukombozi duniani 

Ametoa wito kwa watahiniwa kwenye shule hiyo kujitenga na visa vya utovu wa nidhamu akisema kuwa shule hiyo ndio Mahali pazuri pa kusomea.

Askofu Mkuu Kimengich amekuwa akiongoza halmashauri ya shule hiyo kwa muda wa miaka sita na kwa Sasa wadhifa huo amemkabidhi askofu wa Jimbo katoliki la Kapsabet John Lelei.

Amemkabidhi wadhifa huo askofu amesema kuwa askofu Lelei analeta uzoefu katika maswala ya elimu shuleni humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *