Mwalimu kizimbani

Mwanamme mmoja amefikisha mahakamani Eldoret kwa tuhuma za kumuua mwenzake.

Asbel Kipkoch ambaye ni Mwalimu wa shule ya msingi asemekana kutekeleza kitendo hicho kwa Dennis Kipruto katika eneo la Burudani huko Osorongai Turbo kaunti ya Uasin Gishu wakiwa katika eneo la Burudani kabla yake kumpiga na jiwe kichwani kisa kilichotokea mnamo Januari 11 2026.

Mbele ya hakimu mkuu mwanadamizi wa mahakama hiyo Chesse Cherono Mshukiwa alikana madai hayo.

Mshukiwa akiwasilishwa na wakili Kelvin Korir waliomba mahakama imewachilie mshukiwa na dhamana ambapo mshukiwa aliachiliwa kwa dhamana ya shillingi 500,000 au pesa taslimu ya shillingi 200,000.

Kesi hiyo itatajwa mnamo Aprili 4 2026 huku upande wa mashtaka ukiwa umepanga mashahidi wanne kwenye kesi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *