Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimegich ametilia shaka matumizi ya huduma mpya ya afya ya jamii SHA akisema kuwa bima hiyo imefungua mianya ya watu wachache kupora pesa za wananchi.
Askofu Kimengich amesema kuwa ufisadi nchini ndio umechangia bima hiyo kwa sasa kuonekana kufeli kuwa kuwa wale waliotwikwa jukumu la kutunga sheria na kuwakilisha wananchi katika mabunge yote mawili nchini ndio wamejikita katika visa vya ufisadi.
Amesema kuwa taifa la kenya litapiga hatua kubwa zaidi iwapo visa vya ufisadi vitasitishwa akitoa wito kwa wale ambao wanahudumu katika nyadhifa mbalimbali kujiepusha na tamaa na ubinafsi swala analosema kuwa ndio linalolemaza vita dhidi ya jinamizi la ufisadi nchini.