Askofu Kimengich; Ipo matumaini ya mtumishi wa Mungu Otunga kutawadhwa mwenyeheri

Kumbukumbu ya miaka ishirini na miwili ya mtumishi wa Mungu Maurice Kadinali Otunga imesheheni matumaini na sala ya kumuombea kutawadhwa kuwa mwenyeheri na hatimaye mtakatifu.

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amemmiminia sifa kadinali huyo wa kwanza akitaja kujisadaka kwake bila kujibakisha katika maisha ya sala pamoja na unyenyekevu kama vigezo muhimu ambavyo vitamfanya kutawadhwa kuwa mwenyeheri.

Askofu Kimengich ametoa wito kwa kila mmoja kuiga mfano wa kadinali Otunga akiunga mkono pendekezo la balozi wa baba mtakatifu nchini Bert Van Megen ya kutaka vitabu na nyaraka mbalimbali kusambazwa katika shule za hapa nchini akisema kuwa mchango wake alipokuwa hai hapa nchini ni ushuhuda tosha ambayo kila mmoja anastahili kuiga.

Haya yanajiri baada ya jimbo kuu katoliki la Nairobi kuandaa misa ya kumbukumbu ya miaka ishirini na miwili tangu kufariki kwa mwadhama Maurice Kadinali Otunga, Balozi wa Baba mtakatifu nchini Van Megen akitoa wito kwa wakristu wote wenye nia njema kuwasilisha ushahidi ambayo utapelekea mtumishi huyo wa Mungu kutawadhwa kuwa mwenyeheri na hatimaye mtakatifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *