Wito umetolewa kwa wakristu kutumikia miito yao kwa uaminifu kwa kuwa kila mmoja ametunukiwa miito hizo kama njia moja ya kuimarisha imani yao.
Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amesema kila mmoja ameitwa kutumikia taifa la bwana katika viwango tofauti hivyo haja ya wao kuwa waaminifu na kumruhusu kristu kuwaongoza maishani mwao.
Vilevile amesisitiza haja ya wakristu kando na kushiriki toba katika maisha yao,waweze kuwaombea watumishi katika shamba la bwana kwa kuwa licha ya wao kutoa maisha yao kumfuasi kristu maisha ya yote,wanapitia changamoto si haba,huku akisisitiza ushirikiano baina ya wakristu na watumishi hao ili neno la mungu liweze kuenea kote.