Serikali iko mbioni kuhakikisha kwamba hospitali zote za umma inapata dawa za kutosha na kupunguza mahangaiko ambayo wakenya hupitia wanapotafuta huduma za matibabu kwenye hospitali hizo.
Waziri wa afya Aden Duale alisema kwamba ni sharti serikali zote gatuzi kuweka juhudi za kushirikiana na KEMSA ili kufanikisha upatikanaji wa dawa hizo kwa hosptali zake na kuwapa nafasi wenyeji kupata huduma yenye gharama nafuu.
Duale alikuwa anarejelea pendekezo lake gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim ambaye alitaka kufahamu sababu kuu za serikali za kaunti kukosa dawa za kutosha licha ya KEMSA kupewa mgao wake.
Aidha,seneta wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago amesema kuwa kamati ya afya kwenye bunge la seneti ya kitaifa inashirikiana kuhakikisha sheria na miongozo yote kwenye sekta ya afya inaafikiwa kiukamilifu.