Wizara ya afya katika kaunti ya Pokot Magharibi imeitisha kikao cha dharura na wasimamizi wa afya ili kutathmini hali na kuweka mikakati ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa homa ya nyani (M-pox).
Hii ni kufuatia taarifa ya kudhibitishwa kuwapo kwa kisa kimoja cha ugonjwa wa Mpox katika kaunti ya Trans-Nzoia.
Kulingana na waziri wa afya katika kaunti ya Pokot magharibi Cleah Parklea, wasimamizi wote pamoja na washikadau wa afya wanashauriana kuhusu njia madhubuti ya kukabiliana na hatari ya ugonjwa huo huku suala la kutoa hamasa kwa wakazi likipewa kipaumbele.