Hii si SHA ni tabu tu

Askofu wa jimbo katoliki la Nakuru Cleophas Oseso Tuka ameitaka serikali kuweka sera za kudumu kuhakikisha kwamba sekta ya afya hailegezi kamba kwa shughuli za utoaji huduma kupitia mamlaka ya jamii ya SHA.

Kulingana naye afya ya kila mkenya ni jukumu la serikali kuweka mikakati ya kudumu ili kufanikisha walipa ushuru kuwa wanapokea huduma hizo bila hitilafu yoyote.

Aidha,Askofu Tuka amesisitiza haja ya kila mkenya kuwa mstari wa mbele kuhubiri amani na kuwa na subra wakati wanatekeleza majukumu yao hasa wanapoandamana wahakikishe kuwa wanafanya hivyo bila kuharibu mali ya wengin,au hata kupoteza maisha yaw engine akipiga mfano ya maandamano ambayo hivi majuzi kumeshuhudiwa mauaji,uporaji na uharibifu wa mali,akitilia shaka mafanikio ya uchumi wanchi iwapo hulka hii itaendelea hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *