Serikali ya kaunti ya Elgeyo Marakwet kupitia wizara ya kilimo imetakiwa kuwahamazisha wakulima wa matunda aina ya Passion kuhusu upanzi wa mmea huo.
Haya ni kwa mujibu wa aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Emsoo Christopher Cheboiboch ambaye amesema ukulima wa matunda hiyo ina faida nyingi ikizingatiwa kuwa mkulima huvuna zao hilo kila wiki kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo.