Kamishna wa kaunti ya Trans-Nzoia Sam Ojwang’ amewaonya wakuu wa shule za umma dhidi ya kufuja pesa zilizotengewa miradi ya miundomsingi.
Kwenye kikao na wanahabari mjini Kitale, Ojwang’ amesema kamwe serikali haitawavumilia wakuu hao ambao anasema hushirikiana na wanakandarasi kadhalika bodi za usimamizi ili kufuja pesa hizo. Kamishna huyo aidha amesema wale watakaopatikana wakihujumu mpango wa serikali wa kuimarisha miundomsingi ili kufanikisha asilimia mia moja ya wanafunzi kujiunga na shule za upili, wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.