mwanzo mpya wa matumaini katika Bonde la Kerio unaonekana , Kaunti ya Elgeyo-Marakwet, baada ya Mama Taifa Rachel Ruto kukabidhi nyumba 53 kwa familia zilizoathiriwa na maporomoko ya ardhi yaliyotokea mwezi Oktoba mwaka jana (2025) katika eneo la Chesongoch. Janga hilo la kusikitisha lilichukua maisha ya zaidi ya watu 30 na kuharibu mali na makao ya wakazi wa eneo hilo.
Akizungumza katika eneo la Chesongoch, Eneo Bunge la Marakwet Mashariki, Mama Taifa Rachel Ruto ameeleza kuwa siku ya leo inaleta faraja kubwa na kurejesha tabasamu kwa wakazi hao baada ya kujengewa nyumba hizo kupitia ushirikiano na serikali.
Kando na kukabidhi nyumba hizo, Mama Taifa pia aliwakabidhi waathiriwa hao bidhaa na vifaa muhimu vya matumizi ya nyumbani ili kuwasaidia kuanza maisha upya.
Aidha, Mama Taifa aliweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Rasilimali na Kitovu cha TEHAMA (ICT Hub) cha Chesongoch, hatua inayolenga kupanua fursa za kiuchumi na kielimu kwa wanawake na vijana katika Bonde la Kerio.
