Askofu Kivuva ahimiza demokrasia nchini

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mombasa Martin Kivuva Musonde, ametoa wito kwa wakenya kutokuwa na hofu ya ghasia kuelekea uchaguzi mkuu ujao na badala yake kuombea uchaguzi wa amani.

Akihubiri katika maadhimisho ya misa ya kusherehekea miaka mia moja tangu kufariki kwa mtakatifu Allamano, mbaye ni mwanzilishi wa shirika la Consolata, askofu mkuu Kivuva amesema kuwa kenya ni nchi ya demokrasia, hivyo kila mmoja ana nafasi ya kuwachagua viongozi bila kushurutishwa na yeyote, akisema kuwa uhuru wa kuwachagua viongozi ndio utakaowapa wakenya fursa nzuri ya kuwachagua viongozi waadilifu.

Amesikitishwa na hulka ya wakenya kuwazomea viongozi wanapokuwa kwenye majukwaa mbalimbali, akishtumu kisa ambapo baadhi ya viongozi walizomewa na wananchi kwenye maadhimisho ya sherehe za mashujaa nchini.

Askofu Kivuva hata hivyo ametoa wito kwa viongozi walio mamlakani kuwa na sikio la kuwasikiliza na kutekeleza yale ambayo yanahusu wananchi, kama njia moja ya kupunguza visa vya maandamano na migomo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *