Askofu wa Jimbo katoliki la Nakuru Cleophas Oseso Tuka ametoa wito kwa familia kuwa na msingi dhabiti ili kuwapa malezi Bora vijana.
Akihubiri katika eneo la Kiamunyi Jimbo katoliki la Nakuru askofu Tuka amesema kuwa vijana wengi wamejipata kwenye njia panda kutokana na ukosefu wa uwajibikaji wa wazazi akiwataka wazazi hao siku zote kuwa na wakati na wanao kama njia Moja ya kusikiliza na kutatua changamoto zao.
Askofu Tuka kadhalika ametaka familia hizo kuwafunza wanao Mila na desturi ya ukristu ili kuwapa msingi dhabiti kiimani kwa kuwa Imani hiyo ndio itawasaidia kutambua na kujiepusha na mambo maovu.
