Viongozi wa kisiasa wametakiwa kunadi sera za kiboresha taifa la Kenya badala ya kurushiana cheche za matusi.
Askofu wa Jimbo katoliki la Kapsabet John Lelei amewataka viongozi nchini kukoma kushambuliana kwa kutoa matusi ya kimaumbile akisema kuwa matusi kama hayo ni ishara ya ukosefu wa sera na badala yake ametoa wito kwa viongozi kuangazia sera zitakazowanufaisha wananchi.
Kadhalika askofu Lelei amewataka viongozi wa kisiasa na wanainchi kuwavumilia wapinzani wao kwa kuwapa sikio badala ya kuwafurusha akisema kuwa ukosefu wa kuvumiliana utaleta uhasama hapa nchini.
Kauli sawia na hiyo kadhalika imetolewa na askofu mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria ambaye ametoa wito kwa vijana kuwa waangalifu na wanasiasa walaghai ambao Nia Yao ni kuwatumia kwa maslahi Yao ya kibinafsi.
Amewataka vijana kutafuta mbinu mbalimbali ya kubuni nafasi za ajira badala ya kufadhiliwa na wanasiasa ili kutekeleza visa vya uhuni.
