Viongozi wanawake katika kaunti ya Trans-Nzoia wamewataka wakenya kuendelea kudumisha amani na utangamano ili kutoa mazingira bora ya ukuaji wa uchumi na uetekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Wakiongozwa na aliyekuwa mwakilishi Wadi mteule Naomi Okudo, wametoa wito kwa rais William Ruto kufanya ziara katika kaunti Trans-Nzoia wakihoji kuwa ziara yake imeahirishwa mara kadhaa licha ya wakazi kuwa na matarajio makubwa ya kupata maendeleo zaidi kupitia miradi ya kitaifa.