Waziri wa Usalama wa ndani ya nchi Kipchumba Murkomen, amewashukuru wakaazi wa Bonde la Kerio kwa kurejesha silaha haramu ndani ya kipindi cha makataa yaliyotolewa kwa wamiliki wa silaha hizo kufanya hivyo.
Murkomen hata hivyo amesikitishwa na baadhi ya wakazi wa eneo la Baringo na maeneo mengine ya Kaskazini mwa bonde la Kerio, ambao wamedinda kutii kikamilifu agizo hilo, akiongeza kuwa serikali imeweka mikakati ya kusaidia wanaosalimisha silaha hizo , ikiwemo kuwapa nafasi za kazi kwenye idara mbalimbali za usalama.
Kwa upande wake Naibu Rais Kithure Kindiki ameonyesha matumaini kuwa amani ya kudumu itapatikana hivi karibuni katika Bonde la Kerio, ambapo Hadi sasa, bunduki 285 na risasi 1,953 zimerejeshwa, kauli ambayo imeungwa mkono na viongozi mbalimbali kutoka kaunti hiyo kwenye hafla ya uwezeshaji wa kinamama uliofanyika katika eneo la Sambirir, Marakwet Mashariki kaunti ya Elgeoyo Marakwet.