Wakristu wametakiwa kuwa mstari wa mbele kutetea ukweli na haki katika jamii.
Mwakilishi wa Baba wa baba Mtakatifu nchini Kenya Mwadhama Mathews Herbutus Maria Van Megen alisisitiza haja ya kila mmoja kuwa kielelezo Cha haki katika jamii hasa katika jamii ambayo imejawa na unyanyasaji wa kila wakati.
Akiongea wakati wa maombi ya jioni katika kathedrali ya st.Peter’s Kapsabet,Mwadhama Van Megen alisema kwamba ili jamii kusonga mbele haki,umoja na uwiano yapaswa kuzingatiwa.
Wakati huo,alimtaka askofu mteule wa Kapsabet Yohana Kiplimo Lelei kuiongoza taifa lake bwana kwa njia Bora na kupambana na changamoto ya aina yoyote ili aweze kutimiza agano lake na mwenyezi mungu la kutetea taifa lake Kristu.