Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret John Kiplimo Lelei alitoa wito kwa jamii kusherehekea siku kuu ya krismasi kwa Upendo na kudumisha amani katika familia zao.
Askofu Lelei alisema kuwa huu ni wakati wa familia na jamii kujumuika pamoja na kutafuta maridhiano na kutangamana akitoa wito kwa wakenya kutumia Sherehe hizi za krismasi kudumisha amani.
Askofu kadhalika aliwatakia wakenya wote heri njema za krismasi na mwaka mpya.
