KITUO CHA MAREKEBISHO

Afisa mkuu wa bodi ya kudhibiti vileo na vinywaji kaunti ya Uasin Gishu Koiya Arap Maiyo amesema kwamba,serikali ya kaunti imejitolea kuhakikisha visa vya ulanguzi wa mihadarati imekomeshwa.

Afisa huyo amesema kwa sasa serikali inalenga kujenga kituo kingine cha kurekebisha tabia kwa waathiriwa wa dawa za kulevya ifikapo Januari mwaka ujao.

Aidha,amewataka wakaazi kuendelea kujitokeza na kuwapa mawaidha wanao na pia waathiriwa wa dawa za kulevya ndipo visa hivyo viweze kupungua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *