ASKOFU MUTHAKA; kataeni uaviaji mimba

Askofu wa jimbo katoliki la Garissa George Waithaka amewaonya wakristu dhidi ya kuavya mimba, haswa wakati huu ambapo ripoti za mashirika mbalimbali zinaashiria kuwa kuna idadi kubwa ya wasichana wa shule walio wajawazito.

Akihubiri katika misa ya daraja la upadirisho ya mashemasi watatu wa Abasia ya mfalme wa amani Tigoni, askofu Muthaka amewaonya wale wanaowabagua watoto wanaozaliwa nje ya ndoa, akisema kuwa kadhalika watoto hao wanatoka kwa Mungu, hivyo wanastahili kuonyeshwa upendo kwa kuwa upendo huo kadhalika ni wa Mungu.

Askofu kadhalika amewataka wazazi kuwasaidia wanao kukuza miito mbalimbali na kamwe wasiwashuruitishe wanao kuegemea Miito wasiopendelea, akiwataka siku zote kujenga uhusiano na mwenyezi Mungu kwa kuwa uhusiano huo ndiyo njia ya kipekee ya kukabiliana na changamoto ambazo binadamu hukabiliana nazo kila kukicha.

Misa hiyo kadhalika imehudhuriwa na Abate wa shirika la wabenediktini Abate John Baptist.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *