Vijana wametakiwa kumpa kipaumbele kristu kwa kuwa huyo kristu ndiye mpaji wa vitu vyote.
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri askofu Anthony Muheria, amewataka vijana kumakinikia kristu kwa kusalimisha changamoto zao kwake kristu, haswa wakati huu ambapo kumekuwa na visa vingi vya utovu wa nidhamu miongoni mwa vijana.
Askofu mkuu amesema kuwa suluhu la majanga yote yanayoikumba jamii ni kristu, akitoa wito kwa kila mwanarika kukumbatia sala kama ngao ya kukabiliana na visa vyovyote ambavyo vinaweza kuwa kero katika maisha ya binadamu.
Askofu Muheria aliyasema hayo katika msafara wa vijana kwenye jimbo hilo kauli mbiu ikiwa ni kubelong to JC.
