Askofu wa kiangilikana jimbo la Eldoret Christopher Ruto, amewataka wanasiasa kuwacha kuitilafiana na kazi ya tume Huru na ya mipaka nchini IEBC, wakati taifa linasubiri matokeo ya urais ya uchaguzi mkuu kutangazwa na tume hiyo.
Akiongea katika kanisa la St. Mathew Eldoret, alitaja kuwa tume ya IEBC ina haki ya kutekeleza majukumu yake bila kuingiliwa na yeyote kwa anachosema linafahamu zaidi jukumu lake kwa wananchi.
Askofu Ruto alidokeza kwamba haina haja kwa wanasiasa kueneza semi za uwongo kwa wafuasi wao kuhusu matokeo hayo akiwatahadharisha kwamba hayo huenda yakazua vurugu miongoni mwa wakenya.
Alieleza kwamba wakenya kwa sasa wanapambana na hali ngumu ya maisha na kupanda kwa gharama ya maisha na kunahitajika amani na maelewano.