Wagombeaji watatu wa wadhifa wa ugavana katika kaunti ya Uasin Gishu wametia saini mkataba wa amani na kuahidi kuhubiri na kudumisha amani kabla,wakati na hata baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Viongozi hao Jonathan Bii,Zedikah Bundotich kiprop maarufu Buzeki na William kirwa walisema kwamba wataendesha kampeni zao kwa amani katika muda uliosalia na kuhakikisha wanajiepusha na matamshi ya chuki ili kuwezesha jamii zote kuendelea kuishi kwa utangamano kabla na hata baada ya uchaguzi.
Kwa upande wao viongozi wa kidini na wale wa kibiashara waliozungumza mjini Eldoret waliwataka wagombeaji hao kuzingatia mkataba huo ili maisha yaendelee kama kawaida kwa amani hata baada ya uchaguzi.