Katika tangazo lilitolewa na Baba mtakatifu Leo wa kumi na nne mjini Vatican saa sita mchana ambayo ni saa nane majira ya Afrika mashariki baba mtakatifu ameridhia ombi la askofu mkuu wa jimbo kuu hilo Martin Kivuva la lustaafu na kumteua askofu Kimengich kuwa mrithi wake atakapostaafu.
Wadhifa wa askofu mkuu mwandamizi ina maana askofu Kimengich sasa anakuwa mrithi wa moja kwa moja wa jimbo kuu hilo baada ya kustaafu wa askofu mkuu Kivuva ambaye kufikia tarehe kumi mwezi wa Februari mwaka huu atakuwa amefikia miaka sabini na nne huku umri ya kustaafu kwa askofu ikiwa ni miaka sabini na mitano.
Askofu Kimengich akizungumzia swala hilo ameridhia ombi hilo akisema kuwa ni heshima kubwa ambayo ametunikiwa na mwenyezi Mungu akitoa wito kwa wakristu wa jimbo katoliki la Eldoret alikokuwa mchungaji kwa mud awa miaka sita kumuombea anapochukua jukumu hilo mpya.
Askofu Kimengich alizaliwa mwaka wa 1961 na baada ya masomo ya secondary na masomo ya majiundo ya kikasisi akipata Daraja la upadirisho Septemba kumi na nne mwaka wa 1986 katika jimbo katoliki la Nakuru na kisha baadaye akateuliwa kuwa gombera wa seminary ndogo ya St Josephs kule Molo na kisha baadaye akateuliwa kuwa padre mkuu wa jimbo hilo la Nakuru.
Tarehe 20 mwezi machi mwaka wa 2010 baba mtakatifu Benedikto wa kumi na sita alimteua kuwa askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Lodwar ma kisha baadaye akateuliwa kuwa askofu wa jimbo hilo mwaka moja baadaye.
Mnano mwaka wa 2019 baada ya kifo cha mchungaji wa jimbo katoliki la Eldoret askofu Cornelius Korir baba mtakatifu Francisko alimteua askofu Kimengich kuwa mchungaji wa jimbo katoliki la Eldoret alikokuwa akihudumu hadi kuteuliwa kwake. Katika miaka yake kama mchungaji wa jimbo la Eldoret askofu Kimengich aliasisi kongamano la kwanza la Ekaristia jimboni, kutengenezwa kwa sinodi kubuni maeneo ya kipastorali katika jimbo, maeneo ya sala yakiwemo kabiyet shrine, Burntforest shirine ujenzi was t John amani Centre na kupandishwa hadhi kwa hospitali ya mtakatifu Brigita hadi katika level 4 miongoni mwa mengine mengi
