Majimbo ya Eldoret na Kapsabet sasa wanywa Divai mpya

Jimbo katoliki la Eldoret Sawia na jimbo katoliki la Kapsabet litaanza kutumia ramsi Divai mpya iliyozinduliwa na baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB mwaka ujao.

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amesema kuwa jimbo katoliki la Eldoret litaanza kutumia divai hiyo mpya katika misa rasmi mwaka ujao, akitoa wito kwa wale watakaotaka kununua divai hiyo kufuata taratibu zilizowekwa na baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB, ili kuzuia visa vya divai hiyo kutumika vibaya haswa kama kileo.

Baraza la maaskofu liliweka sheria kwamba yeyote atakayetaka kununua divai hiyo, sharti atafute idhini kutoka kwa askofu au padre anayehusika, na kwamba sharti atakuwa na hati ambayo itaonyesha kuwa ameidhinishwa kununua divai hiyo.

Divai hiyo kadhalika haitauzwa katika maduka ya jumla kama ilivyokuwa ikiuzwa ya hapo awali, na kwamba majimbo yataagiza divai hiyo moja kwa moja kutoka katika taifa la afrika kusini.

Hatua sawia na hii kadhalika imechukuliwa na  jimbo katoliki la Kapsabet, askofu wa jimbo hilo Yohane Lelei akidokeza kuwa tayari jimbo hilo limeweka mikakati ya kuona kuwa divai hiyo, inawafikia wakristu wa jimbo hilo katika parokia mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *