Wakazi wa kijiji cha Kapkakaa, katika wadi ya Emsoo, Kaunti ya Elgeyo Marakwet, wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa maji safi eneo hilo.
Mwakilishi wa wadi hiyo, Christopher Cheboiboch, aliyeongoza hafla hiyo, amewahimiza wakazi kutumia vyema rasilimali hiyo muhimu kwa matumizi yao ya nyumbani na pia kuendeleza shughuli za kilimo cha unyunyiziaji mashamba kama njia bora ya kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wao, wakazi wa eneo hilo wakiongozwa na Sally Kiplagat na Herman Kwambai, wameelezea furaha yao wakisema kuwa mradi huo ni afueni ikizingatiwa changamoto ambazo wamepitia kutafuta maji kwa muda mrefu.
