Baba Mtakatifu Leo wa kumi na nne amewataka waumini kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa Amani na ujirani mwema kama njia muafaka wa kukabiliana na madhila na nynyaso mbalimbali duniani.
Kulingana naye vita baina ya mataifa na hata za wenyewe kwa wenyewe yameathiri kwa kiwango kikubwa maendeleo endelevu miongoni wa wananchi wengi wakipoteza makao wakiwemo kina mama na watoto swala analosema linakwenda kinyume na utu na ubinadamu, akikariri kuwa njia ya kukomesha vita hivi ni kila mmoja kuwa balozi wa amani.
Amesema kwamba viongozi duniani wanapaswa kuweka chini silaha kali na kukumbatia mwito wa Amani huku akisikitikia vita vinavoshuhudiwa katika mataifa kama vile Ukraine,Urusi.
