Changamoto hizo ziwe nguvu zako

Wakristu wametahadharishwa dhidi ya kukata tamaa kwa kuwa hulka hiyo hulemaza maswala mengi katika maisha ya binadamu.

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Subira Anyolo ametoa wito kwa kila mmoja kamwe kutopoteza matumaini kwa kuwa Mungu yupo, na anatazama kila changamoto ya kila mmoja, akisema kuwa kila changamojo huashiria mateso ya yesu msalabani, ambayo ndio chemichemi ya ukombozi wa kila binadamu.

Askofu kadhalika alisema kuwa kumtegemea mwenyezi Mungu katika kila jambo huwapa nguvu ya kukabiliana na misukosuko ya dunia hii ambayo imejaa kelele nyingi, akitoa wito kwa kila mmoja kuwa na hulka ya kuzungumza na Mungu kupitia sala  ili awanasue na changamoto ibuka.

Alitoa wito kwa kila moja kuwa karibu na mwenyezi Mungu kwa kuwa ukaribu huo, huja na neema na karama kutoka kwa mwenyezi Mungu ambayo huwapa matumaini na nguvu ya kukabiliana na changamoto hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *