Papa Leo XIV awatangaza Watakatifu wapya Carlo Acutis na Pier Giorgio

Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza ibada ya Misa takatifu na kuwatangaza walei vijana wawili kuwa watakatifu.

Mtakatifu Carlo Acutis alikuwa kijana mdogo mwenye umri wa miaka kumi na sita aliyetumia mitandao na teknolojia kueneza habari njema ya kristu kabla ya kufariki kutokana na ugonjwa wa leukemia.

Papa Leo wa kumi na nne akitoa tangazo hilo ametoa wito kwa vijana wa karne hii kuwa makini na matumizi ya mitandao akisema kuwa vijana wana nafasi ya kutumia mitandao kueneza injili, kukuza mazingira na hata kujihusisha na maswala ya maendeleo endelevu katika jamii.

Pier Giorgio naye alikutana na Bwana kupitia shule na vikundi vya Kanis, Chama cha Matendo ya Vijana Katoliki, Mkutano wa Mtakatifu Vincent wa Paulo, Shirikisho la Vyuo Vikuu Katoliki Italia (FUCI), na Udugu wa tatu wa Wadominikani na alishuhudia hili kwa furaha yake ya maisha na maisha yake ya Kikristo.

kwa njia ya sala, urafiki, na mapendo. Kiasi kwamba, walipomwona akizunguka katika mitaa ya Torino  na mikokoteni iliyojaa misaada kwa maskini .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *