Ombi la kubuniwa kwa Jimbo katoliki la Kapsabet limekuwa ni ruwaza ya marehemu askofu Cornelius Korir.
Askofu wa Jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich akihubiri katika misa ya shukrani ya kwanza ya askofu wa Jimbo Katoliki la Kapsabet katika kathedrali ya mtakatifu Petero mjini Kapsabet, askofu Kimengich alisema kuwa ruwaza wa kuanzishwa kwa jimbo hilo lilipitia ombi la askofu marehemu Cornelius Korir pamoja na wakristu wengine wa jimbo hilo akisema kuwa ombi hilo lilitimia Jumamosi baada ya kuwekwa wakfu.
Askofu alisema kuwa jimbo hilo kadhalika linajivunia maswala mengi ikiwemo eneo la Sala la Kabiyet parokia mbalimbali pamoja na mapadre hamsini na moja na miito mbalimbali kama sababu ambazo zimepelekea kubuniwa kwa Jimbo katoliki la Kapsabet.
Askofu Kimengich alimsifia askofu mwanzilishi wa jimbo hilo John Kiplimo Lelei kwa weledi na tajiriba katika kazi yake akisema kuwa ana Imani na utendakazi wake akitoa wito kwa mapadre kumuunga mkono katika kazi hiyo ya kichungaji.