Huzuni imetanda katika kijiji cha Tenderwa katika eneo la Kapyego kaunti ndogo ya marakwet Mashariki kaunti ya elgeyo marakwet baada mwanamke mmoja kufariki baada ya kupigwa na radi jioni wa kuamkia leo.
Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi katika kaunti hiyo Peter Mulinge amesema kuwa mwendazake Jackline warakera mwenye umri wa miaka 35 alipigwa na radi alipokuwa akijikinga mvua chini ya mti.
Kamanda huyo ameongeza kuwa baada ya kisa hicho mwathiriwa alikimbizwa kupokea matibabu katika kituo cha afya cha Kapyego na kuthibitishwa kuwa amefariki alipofika.
Hata hivyo mwili wa mwendazake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya misheni ya Kapsowar.