Mumezidi na kutuchotea Maze

Wafanyibiashara katika jiji la Eldoret walisema wanakadiria mamilioni ya pesa kutokana na kufungwa kwa biashara siku ya jumatatu kuadhimisha miaka 35 ya Saba saba ya upatikanaji wa uhuru wa vyama vingi nchini.

Wakizungumza na wanahabari jijini Eldoret,wafanyibiashara hao wanasikitikia kile walisema maswala ya kiuchumi isipochukuliwa kwa umakini kwa wakenya na kuhakikisha wanapoandamana wanaandamana kwa Amani,taifa haliwezi kusonga mbele.

Wamesema licha ya jiji la Eldoret kushuhudia utulivu,walidhamiria kuendelea na biashara yao ila kutokana na uwoga waliokuwa nao kuwa huenda waporaji wakavamia maduka zao na hivyo kutaka wakenya kuwa uwiano na mshikamano miongoni mwao maana wao wote ni ndugu.

Maandamano ya Saba Saba huadhimishwa kila mwaka kutokana kuidhinishwa kwa kipengee cha pili cha katiba ambayo inaruhusu taifa kuwa na vyama zaidi ya moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *