Hafla ya kuapishwa kwa James Nyoro kama gavana wa tatu wa kaunti ya Kiambu imehairishwa. Taarifa kutoka kwa idara ya mahakama inasema uamuzi huo umeafikiwa baada ya mashauriano ya kina.Hafla hiyo iliratibiwa kufanyika leo ili Nyoro kuchukua nafasi ilioachwa wazi na Ferdinand Waititu aliyebanduliwa afisini hapo jana.