Askofu mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Mombasa Martin Kivuva Musonde amekaribisha uteuzi wa askofu Dominic Kimengich kuwa askofu mwandamizi mteule wa Jimbo hilo.
Askofu mkuu Kivuva amebaini kuwa uteuzi huu wa askofu Kimengich ulirudhia ombi lake la kutaka kustaafu akimtaja kama mchapakazi ambaye ameongoza majimbo mawili na kadhalika kuwa mkunga wakati wa kuzaliwa kwa Jimbo katoliki la Kapsabet miongoni mwa mengine.
Ametoa wito kwa wakristu wa Jimbo kuu katoliki la Mombasa kumkaribisha askofu mkuu mwandamizi mteule na kumpa makaribisho mazuri akisema kuwa askofu mkuu mwandamizi mteule Kimengich analeta uzoefu wa hali ya juu kwa kuwa ana uweledi katika maswala ya Sheria za kanisa akitoa wito kwa wakristu wa Mombasa kutombagua kwa msingi wa kikabila na Mahali anakotoka.
