Kanisa lafungua tena hospitali ya St Mary’s

Askofu wa jimbo katoliki la Kakamega Joseph Obanyi Sagwe ametangaza rasmi kufunguliwa tena kwa hospitali ya kimehseni ya St Marys Mumias ambayo ilikuwa imefungwa tangu mwaka jana kufuatia mgomo wa wahudumu wa afya.

hospitali hiyo ilifungwa mwaka jana baada ya usimamizi kudai kucheleweshwa kwa malipo ya bima ya afya ya jamii SHA, askofu Obanyi akisema kuwa wamelazimika kukopa fedha ili hospitali hiyo iweze kumudu mahitaji yake na kufunguliwa mwishoni mwa mwezi.

askofu hata hivyo amesema kuwa hospitali hiyo itafunguliwa kwa awamu kabla ya kuanza kiukamilifu ili kuhakikisha kuwa huduma zake zote ziko katika hali sawa ya kuwahudumia jamii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *