Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ametaoa wito kwa wakristu wa jimbo kuendelea kuhuburi ujumbe wa matumaini licha ya mwaka wa jubilei kuelekea kufika ukingoni.
Askofu Kimengich amesema kuwa matendo ya matumaini ni dhihirisho ya upendo wao kwa mwenyezi Mungu akitoa wito kwa kila mmoja kamwe kutochoka kuhubiri habari njema na kuwapa matumaini wale waliokata tamaa maishani.
Ametoa wito wa umoja ya wanajimbo akiwataka siku zote kudumu katika sala, ambayo anasema kuwa humjalia kila mmoja karama kutoka kwa mwenyezi Mungu.
Askofu kimengich kadhalika amesema kuwa mwaka huu wa jubilei ambayo ilinogeshwa kwenye kauli mbiu mahujaji ya matumaini, ilileta mafanikio makubwa katika jimbo ikiwemo kupatikana kwa jimbo jipya la Kapsabet na zawadi ya miito mbalimbali jimboni.
