Wakulima katika kaunti ya Uasin Gishu wamehimizwa kukumbatia ufugaji wa samaki kando na kilimo cha mimea mbalimbali ili kujiongezea mapato.
Kulingana na mtaalamu wa kilimo cha samaki kaunti hiyo Lina Onsari, alielezea kuwepo kwa rasilimali za majini ambazo hazitumiwi akiwataka wakulima kujitosa kwenye kilimo hicho.
Onsari alieleza umuhimu wa wakulima kutumia mabwawa ya nyumbani kukuza samaki kwa usalama wao kiafya ikizingatiwa kuwa maziwa na mito inaendelea kuchafuliwa na shughuli za kibinadamu.
Wakati uo huo alitaja uwepo wa soko tayari la samaki katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo kaunti ya Uasin Gishu na hivyo mkulima anahakikishiwa faida.