Kilimo ndani ya UDA

Aliyekuwa mbunge wa Marakwet Mahariki Linah Chebii Kilimo amejitoza siasani tena mara hii akijiunga na chama cha United Democratic Alliance.

Akizungumza jijini Eldoret wakati wa mkutano uliowaleta pamoja viongozi mbalimbali wa UDA ukanda wa North Rift,Chebii alisisitiza kwamba amekua gizani kwa muda mrefu sasa na kujiunga kwake na chama hicho tawala huenda akapata nafasi ya kuleta mchango wake hasa kuhusiana na maswala yanayowakumba wenyeji eneo la Kerio Valley ambapo tangu jadi kumeshuhudiwa utovu wa usalama.

Kwa upande wake,katibu mkuu wa UDA Omar Hassan amepongeza hatua hiyo akiwataka viongozi kutoka pembe zote nchini kuiga mfano wa waliowatangulia kujiunga na serikali akieleza kwamba umoja wa nchi ndio silaha pekee ya maendeleo.

Yamejiri hata wakati na ambapo,kiongozi wa chama cha KANU Gideon Moi naye alitii na kubali kujiunga na serikali mkutano uliofanyika eneo la Kabarak,huku rais akiwa amefanikiwa kuwanasa wanasiasa wakuu wawili sasa wa kwanza akiwa kinara wa ODM Raila Odinga ambaye yuko kwenye serikali jumuishi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *