Ualimu taaluma bora zaidi uadilifu ikitangulia

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ametoa wito kwa walimu kuwa waadilifu katika taaluma yao, akisema kuwa ukosefu wa uadilifu utazamisha merikebu ya elimu na hivyo kukuza kizazi kisicho na mwelekeo.

Akihubiri katika misa ya kuadhimisha jubilee ya walimu kwenye kanisa la moyo mtakatifu wa Yesu kathedrali, askofu Kimengich aliwataka walimu wakuu pamoja na walimu kufahamu kuwa ualimu ni zawadi kutoka kwa mwenyezi Mungu, akitoa wito kwa walimu hao kuwaongoza wanafunzi kwa njia ya uwazi na uadilifu.

Aliwataka walimu na wanafunzi siku zote kutembea na kristu katika kila jambo, akiwahimiza kutenga  nyakati maalum ya sala katika shule mbalimbali, kwa kuwa kristu ndiye nguvu na ngao ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.

Askofu kadhalika aliwahimiza walimu wanaoongoza shule zinazomilikiwa na kanisa katoliki, kuweka bidii zaidi na kuwaongoza wanafunzi kwa hekima ili kizazi kijacho kiwe na watu wa kutegemewa katika jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *