Acheni majigambo dunia duara tu i say

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria amewakanya wakristu dhidi ya kujigamba licha ya vyeo walivyo navyo  katika jamii kwa kuwa ni nguvu kutoka kwa mwenyezi Mungu.

Akihubiri katika misa ya kusherehekea jubilee ya miaka ishirini na tano ya watawa wa shirika la mtakatifu yosefu wa Trabes jimboni humo, askofu mkuu Muheria amesema kuwa njia mwafaka wa kudhihirisha ukuu wa Mungu katika maisha ni kuwa na ukarimu, unyenyekevu, kuwajali wale waliokata tamaa katika jamii badala ya kujigamba.

Askofu Muheria kadhalika alisema kuwa uchoyo kiburi na majigambo sio matunda ya roho mtakatifu, akitaka kila mmoja kujirudia na kukumbatia unyenyekevu na uchaji wa Mungu siku zote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *