Mahakama ya Eldoret imeamuru mwanamke mmoja anayetuhumiwa kuiba mtoto azuiliwe kwa siku 21 katika kituo cha polisi cha langas ili kufanikisha shughuli za maafisa wa polisi kukamilisha uchunguzi wao.
Monica Kwamboka anadaiwa kumiba mtoto huyo wa miaka 6 mnamo tarehe 18/5/2024 katika mtaa wa langas kabla ya kupatikana katika kaunti ya Kisii.
Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kwamba, mtoto huyo alitoweka kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kupatikana tarehe 6/10/2025 ambapo mahakama ilielezwa kwamba tayari mtoto huyo alikua ameingizwa katika shule ya msingi ya Nyakeiyo na mshukiwa huyo akiwa katika gredi ya kwanza.
Mshukiwa huyo bila ya pingamizi yoyote,alisema yuko tayari kumleta mahakamani yule ambaye alimuuzia mtoto huyo kwa shilingi 30,500
Kwamboka aliiambia mahakama kwamba alifukuzwa alikokuwa ameolewa baada ya kukosa kupata mtoto na aliporejea nyumbani akapoteza mamake na ndiposa shangazi yake akamshauri atafute mtoto waishi naye kwenye boma hilo chanzo Cha yeye kushirikiana na mwenye kumuiba mtoto amuzie mtoto huyo.
Mahakama imeagiza mtoto huyo aendelee kukaa katika katika makao ya watoto jijini Eldoret hadi uchunguzi wa DNA kati yake na mamake pamoja na mshukiwa huyo uweze kufanyika.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 29/10/2025.