Wito huu isonge mbele zaidi

Wakuu wa mashirika mbalimbali za kitawa wametakiwa kuwa na uvumilivu wanapowaongoza watawa wa mashirika yao.

Askofu wa jimbo katoliki la Lodwar John Mbinda akihubiri katika misa ya kufunga warsha iliyowaleta pamoja wakuu wa mashirika mbalimbali hapa nchini, amesema kuwa kuongoza mashirika hayo yanahitaji uvumilivu na sala kwa kuwa wanawaongoza wale wanaohamu ya kumtumikia kristu na changamoto mbalimbali.

Aliwataka daima dawamu kutokata tamaa katika jukumu hilo na badala yake wapalilie tunda la matumaini katika jukumu lao ikizingatiwa kuwa kwa sasa kuna changamoto ibuka katika pembe zote za dunia akitoa wito kwao kujisadaka bila kujibakisha katika majukumu hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *