Uinjilishaji iendelee au sio

Askofu wa Jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amefanya teuzi katika parokia mbalimbali katika juhudi za kuimarisha shughuli za uinjilishaji jimboni.

Katika teuzi hizo askofu Kimengich amemteua padre Hillary Nyongi aliyekuwa akihudumu kama paroko wa parokia ya Mogil kuwa padre msaidizi katika kanisa la moyo mtakatifu wa yesu kathedrali, padre Geoffrey Simali aliteuliwa kuwa paroko wa parokia mpya ya St Josephine Bakita Lower Moiben, padre John Aluodo ametumwa kuhudumu katika parokia ya malaika wakuu Koibarak naye Daniel Laboso akitumwa kuhudumu katika parokia ya Mogil.

Askofu kadhalika amekweza kituo cha mtakatifu Monica Emkwen kuwa parokia na kumteua padre Elphas Talam kuwa paroko wa parokia hiyo mpya .

Askofu kadhalika amewaalika wakristu wote kwenye Misa ya kumbukumbu ya nane ya askofu nwendazake Cornelius Korir tarehe thelathini mwezi huu wa oktoba kwenye kanisa la moyo mtakatifu wa yesu kathedrali kuanzia saa saba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *