Tambua mwanao vyema

Wito umetolewa kwa wazazi kuwa karibu na wanao ili wasije wakajiingiza kwenye vikundi vya watoto watundu likizo ya Aprili ukiwa umewadia.

Kulingana na askofu mteule wa jimbo katoliki la Eldoret  Monsinyo John Kiplimo Lelei  ni kuwa, jukumu la kila mzazi ni kuhakikisha wanatambua wanao vyema kitabia ndipo wasije wakajipata katika njia panda ya kuwa waraibu wa mihadarati.

Alisema kwamba wazazi wengi walitelekeza majukumu yao swala linalochangia vijana wengi kuwa na utovu wa nidhamu akitaka hili kukomeshwa.

Aidha,Monsinyo Kiplimo Lelei aliwataka wanafunzi nao kutowaogopa wazazi wao na kuwa wa wazi kwa wazazi wao ndio waweze kusaidia kutatua changamoto ambazo huenda wanapitia maishani mwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *