Njia msalaba kwenye bonde la mauti

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Domonic Kimengich ameongoza njia ya msalaba katika eneo la Endo kaunti ya Elgeiyo marakwet akitoa wito kwa wakaazi wa eneo hilo kuendelea kudumisha amani.

Askofu amesema kuwa lengo la njia ya msalaba katika eneo hilo la Endo ni kuombea amani haswa kwa wakaazi wa eneo hilo, ambalo linakumbwa na machafuko kila kukicha kutokana na wezi wa mifugo, akiwapa ujumbe wa matumaini kuwa mwenyezi Mungu atawapa suluhu la kudumu.

Kadhalika askofu  amezifariji familia ambazo zimepoteza familia zao katika maeneo ya Liter, Sambalat ambazo zilipoteza wapendwa wao katika machafuko yanayoshuhudiwa katika maeneo hayo , na kuwataka kusalia watulivu.

INSERT LITER

Haya yanajiri baada ya watu wawili kupata majeraha mabaya huku mifugo zikiibwa usiku wa kuamkia leo katika katika eneo la Mogil kaunti hiyo ya Elgeiyo Marakwet.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *