kanisa lakosoa serikali kutokan na ufisadi

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mombasa Martin Kivuva Musonde ametoa wito kwa serikali kutathmini kwa mara nyingine ushuru unaotozwa wakenya akisema kuwa unawasakama wakenya.

Katika ujumbe wake wa pasaka katika kathdrali ya Holy cross jijini Mombasa askofu mkuu Kivuva amesema kuwa serikali na idara husika za kupigana na ufisadi inastahili kuweka mbinu mwafaka wa kukabiliana na ufisadi badala ya kuwatoza wakenya ushuru ambayo anasema unawazamisha wakenya kwenye lindi la umaskini.

Ametaka tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC kukoma kunyosha kidole cha lawama kwa idara ya serikali bali ichukulie hatua wahusika wote na kutwaa mali yote yaumma iliyoporwa .

Hata hivyo ametoa wito kwa rais William Ruto kukoma kukopa pesa nyingi katika mataifa ya kigeni akisema kuwa hatua hiyo inawapa wakenya mizigo mizito akiwataka viongozi kubuni nafasi nyingi za ajira kama njia moja ya kufufua uchumu wa taifa hili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *